Siku mbili mfululizo (Jumamosi na Jumapili) Tanden iliwakilisha Tanzania katika maonyesho ya Afrika messen 2018, ambayo yalifanyika katika manispaa ya Gladsaxe.
Maonyesho hayo ambayo lengo lake kubwa ni kuonyesha picha halisi ya Afrika kwa hapa Denmark katika nyanja mbalimbali (Biashara, asasi zisizo za kiserikali na watu binafsi) ambao wote walikua wanawakilisha nchi zao. Viongozi wa juu wa Tanden na baadhi ya wanachama waliweza shirikiana bega kwa bega katika kupeperusha bendera ya Tanzania.
Katika banda la Tanzania kulikua na bidhaa mablimbali kutoka Tanzania kama (nguo,shanga,viatu,viuongo vya chakula n.k). Mauzo yaliyopatikana yanakwenda kusaidia moja kwa moja Tanzania katika asasi ya wakasa- Arusha pamoja na kuingia kwenye mfuko wa pesa wa Tanden.
Baadhi ya watu na wateja waliofika katika banda la Tanzania walitoa maoni yao mbalimbali katika uwakilishi wa Tanzania katika maonyesho mengine kama hayo,
"Tunahitaji bidhaa nyingi zaidi kuliko zilizopo hapa, mfano kahawa toka Tanzania,korosho,shanga n.k"
Tanden pia inapenda kuwasihi watanzania ambao wanaishi hapapindi inapotokea fursa kama hii ama kitu chochote ambacho kitatambulisha nchi yetu ya Tanzania ni vizuri watu wakajitokeza na kupeana habari zaidi na kushauriana ni vipi Tanzania, inaweza wakilishwa kwa upana zaidi katika nyanza nyingi tofauti.
Pia Tanden inapenda kuwashukuru wale wopte walio jitolea kwa hali na mali katika kufanikisha Afrika messen 2018 kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania, licha ya ugumu uliojitokeza kwa siku zote mbili.
"UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI DHAIFU"