Habari hii ni kutoka Ubalozi wa Tanzania Sweden
Kwa Jumuia za Diaspora ya Watanzania
Kwa Jumuia za Diaspora ya Watanzania
Ubalozi umepokea barua kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Tanzania kuhusu maombi ya Ardhi kwa ajili ya Uwekezaji kwa watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).
Barua hiyo inafahamisha kwamba Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tanzania, inakaribisha maombi ya Ardhi ya Uwekezaji kwa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).
Kwa wale wanaopenda kuomba ardhi kwa ajili ya uwekezaji, Tanzania tafadhali tumeni maombi kwa;
Ofisi ya Kamishna wa Ardhi
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tanzania
K.K . Mh. Balozi
Ubalozi wa Tanzania
Sweden
Barua za maombi zitumwe kupitia Ubalozini.
Katika maombi haya itafaa ikiwa mwombaji ataeleza mkoa/wilaya ambayo ardhi hii inahitajika, ukubwa wa ardhi na dhumuni au matumizi yanayotarajiwa.
Zoezi hili ni endelevu hivyo mnahamasishwa kutuma maombi yenu kwa kadri mtakavyoweza.
Ubalozi wa Tanzania
Stockholm
Leave a Reply