"Diaspora wana nia ya kuisaidia nchi yao"
"Uelewa wa matatizo yaliyopo na kukubali hali tofauti na kuendeleza upembuzi yakinifu na vitendo kwa ufumbuzi. Yote hii inakuja kutokana na uzoefu wa pamoja wa Diaspora na jamii." Tengo Kilumanga
Katika kuendeleza gurudumu la uwelewa wa diaspora kwa Tanzania na ugenini "Denmark", Tanden itafanya kikao siku ya jumamosi ya tarehe 04-02-2017 kuanzia saa sita za mchana mahala Frode Jakobsens Plads 4, 1.sal Vanløse.
Njoo tuzungumzie mambo ya diaspora na sheria ya umiliki wa ardhi Tanzania.
- Nini maoni yako
- Nini kifanyike
- N.K
Tukitaka kuelewesha umma wa Tanzania na hata hapa ughaibuni, diaspora inatoa mchango gani, basi inatupasa tuwe na sauti moja na kuonyesha kwa vitendo ni mchango gani wana diaspora wanachangia nyumbani "Tanzania" .
NJOO TUZUNGUMZE KWA PAMOJA SIKU YA JUMAMOSI YA 04-02-2017, KARIBU KATIKA MKUTANO KWAAJILI YA KUZUNGUMZIA MAMBO YA DIASPORA.