-
Katiba Yetu
KATIBA YA TANZANIA DENMARK ASSOCIATION (TANDEN)
SEHEMU YA KWANZA: JINA NA MADHUMUNI
1. Jina la Chama litakuwa Tanzania Denmark Association, kwa kifupi TANDEN.
2. Makao Makuu ya TANDEN yatakuwa Copenhagen
3. Kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya TANDEN yatakuwa yafuatayo:-
(a) Kuwaunganisha na kuwakutanisha watanzania waishio hapa Denmark bila kujali dini zao, itikadi zao za kisiasa, au kabila zao.
(b) Kuyapa kipaumbele mambo muhimu yanayohusu maendeleo ya nchi yetu katika nyanja mbalimbali kama vile Elimu, Afya, Uwekezaji, Utalii, Ustawi wa jamii n.k.SEHEMU YA PILI: UANACHAMA
I: Masharti ya uanachama:
Mtu yeyote anaruhusiwa kuwa mwanachama wa TANDEN kama atatimiza masharti yafuatayo:
1. Raia yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 16
Tunaposema raia wa Tanzania tunamaanisha:
• mtanzania mwenye uraia wa kuzaliwa (mzalendo).
• mtanzania mwenye uraia wa kuandikishwa.
2. Mtu yeyote asiyekuwa raia wa Tanzania ataruhusiwa kuwa mwanachama wa TANDEN kama atatimiza masharti yafuatao
• alikuwa na uraia wa au asili ya Tanzania pamoja na kwamba hivi sasa ana uraia wa nchi nyingine
• mtoto ambaye mzazi/wazazi wake wana asili ya Tanzania hata kama watakuwa na uraia wa nchi nyingine
3. Atatoa kiingilio cha Uanachama
4. Atalipa ada ya mwaka ya Uanachama
5. Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa na chamaII: Utaratibu wa kuomba Uanachama, Kiingilio na Ada za Uanachama
(1) Mtu yeyote anayependa kujiunga na TANDEN anakaribishwa kupeleka maombi yake kupitia kwa viongozi wa TANDEN
(2) Kamati kuu ya TANDEN itakaa chini na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya uanachama.
(3) Mtu akikubali kuwa mwanachama wa TANDEN itabibi atekeleze yafuatayo
(i) Atatoa kiingilio cha uanachama ambacho ni kroner 50
(ii) Atalipa ada ya unanachama kwa mwaka ambayo ni kroner 100
(iii) Atatoa michango yote iatakayokubaliwa na chama
(4) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na kamati kuu ya TANDEN.III: Kikomo cha Uanachama
Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a) Kujiuzulu mwenyewe
(b) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba
(c) Kutotimiza masharti ya uanachama kama yalivyotajwa katika sehemu ya pili hapo juuIV: Kujitoa Uwanachama
(1) Mwanachama anaweza kujitoa kwenye chama wakati wowote ule kwa hiari yake mwenyewe kwa kuandika barua kwa viongozi wa chama
(2) Wanachama wa TANDEN wanaweza kumwondoa mwanachama mwenzao kama wakiona kuwa mwanachama huyo ameshindwa kutimiza masharti ya uananachama e.g. kutolipa ada ya mwaka, michango ya chama, kutoshiriki katika shughuli za chama
(3) Mwanachama ambaye uanachama wake umekwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
(4) Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka kuingia tena katika chama, itabidi aombe upya na atapeleka maombi yake kwa viongozi wa TANDEN
(5) Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika TANDEN ataomba upya kujiunga na chama kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanachama kwa mujibu wa Katiba ya TANDEN.V: Haki za mwanachama
Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo:-
(1) Haki ya kushiriki katika shughuli zote za TANDEN kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
(2) Haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake katika mikutano ya TANDEN pale ambapo anahusika kwa mujibu wa Katiba.
(3) Haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa TANDEN na ya kuchagua viongozi wake kwa mujibu wa katiba ya TANDEN
(4) Haki ya kujitetea au kutoa maelezo yake mbele ya Kikao cha TANDEN kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake, pamoja na haki ya kukata rufani ya kwenda katika Kikao cha juu zaidi cha TANDEN kama kipo endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa.SEHEMU YA TATU: VIONGOZI
I: Sifa za kiongozi
(1) Wawili kati ya viongozi wakuu wa TANDEN ni lazima wawe wamekaa hapa Denmark muda usiopungua miaka mitatu (3) na wanaweza kuongea kidenish.Uongozi wa kiongozi utakoma kwa:-
(a) Kujiuzulu mwenyewe.
(b) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(c) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.(2) Kiongozi aliyeachishwa au kufukuzwa uongozi anaweza kuomba tena nafasi ya uongozi wowote na maombi yake yatafikiriwa na kutolewa uamuzi na kikao kilichomwachisha au kumfukuza uongozi.
(3) Mwanachama anayeomba nafasi ya uongozi wa aina yoyote katika TANDEN
hatakubaliwa kuwa amechaguliwa mpaka awe amepata zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.
(4) Katika uchaguzi wa kujaza nafasi nyingi kwa pamoja, ushindi utahesabiwa kwa kufuata wingi wa kura alizopata mwombaji wa nafasi hiyo zaidi ya wenzake, bila kujali kama kura hizi zinafikia nusu ya kura halali zilizopigwa.
S NNE AO VYA TAIFA
II: Viongozi wakuu wa TANDEN
1. Mwenyekiti:
• Atachaguliwa na mkutano mkuu wa TANDEN na atakuwa kwenye nafasi hiyo ya uongozi kwa muda wa miaka 2 lakini anaweza kuchaguliwa tena mara moja baada ya muda huo kumalizika. Baada ya kuwa madarakani kwa awamu mbili, kiongozi hataruhusiwa kugombea mpaka iwe imepita awamu moja bila yeye kuwa madarakani.
• Atakuwa mwenyekiti wa mkutano mkutano TANDEN, Kamati kuu ya TANDEN
• Mwakilishi mkuu wa TANDEN
• Katika mikutano yote anayoiongoza, zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida mwenyekiti atakuwa na kura ya uamuzi endapo kura za wajumbe walioafiki na kutoafikiana zitalingana.2. Katibu:
a. Atachaguliwa na mkutano mkuu wa TANDEN na atakuwa kwenye nafasi hiyo ya uongozi kwa muda wa miaka 2, lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika. Baada ya kuwa madarakani kwa awamu mbili, kiongozi hataruhusiwa kugombea mpaka iwe imepita awamu moja bila yeye kuwa madarakani.
b. Atakuwa katibu wa mkutano mkuu wa TANDEN, Kamati kuu ya TANDEN
• Atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa TANDEN na atafanyakazi chini ya uongozi wa Kamati kuu ya TANDEN.
• Atakuwa na jukumu la kuitisha mkutano mkuu wa TANDEN, Kamati kuu ya TANDEN.
• Kuandika mhitasari wa vikao vyote vya TANDEN na kutunza kumbukumbu za mikutano yote ya TANDEN.3. Mwekahazina
• Atachaguliwa na mkutano mkuu wa TANDEN na atakuwa kwenye nafasi hiyo ya uongozi kwa muda wa miaka 2, lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika. Baada ya kuwa madarakani kwa awamu mbili, kiongozi hataruhusiwa kugombea mpaka iwe imepita awamu moja bila yeye kuwa madarakani.
• Atakuwa ndiye msimamizi ya masuala yote ya uchumi na fedha na mali za chama
• Atatoa taarifa zote kuhusu mapato na matumizi ya chama
• Atatakiwa kuleta majina ya wanachama ambao hawajalipa ada zao za mwaka kwenye kikao cha kamati kuu ya TANDENSEHEMU YA NNE VIKAO VYA CHAMA
I: TANDEN itakuwa na Vikao vifuatavyo:
(1) Mkutano Mkuu wa TANDEN
(2) Kamati Kuu ya TANDEN
(3) Mkutano wa dharuraMkutano Mkuu wa TANDEN utakuwa ndicho Kikao Kikuu cha TANDEN kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho.
Mkutano Mkuu wa TANDEN utafanya mikutano yake ya kawaida mara mbili kwa mwaka. Mikutano huu utafanyika wiki ya pili ya mwezi Mei na wiki ya pili ya mwezi Novemba . Lakini mkutano usiokuwa wa kawaida (dharura) unaweza kufanyika wakati wowote ukiitwa na Mwenyekiti wa TANDEN au ukiombwa na theluthi mbili ya wanachama wote wa TANDEN.Taarifa ya Mkutano Mkuu wa TANDEN ni lazima itolewe si chini ya mwezi mmoja kabla ya tarehe ya kukutana. Lakini inaweza kutolewa taarifa ya muda mfupi zaidi ya huo ikiwa unafanyika mkutano usiokuwa wa kawaida (dharura).
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa TANDEN atakuwa ni Mwenyekiti wa TANDEN na asipoweza kuhudhuria, mmoja wa viongozi wakuu yaani katibu au mweka hazina ataongoza Mkutano huo. Iwapo itatokea kwamba wote watatu hawawezi kuhudhuria Mkutano huo, Kamati Kuu ya TANDEN itamchagua Mjumbe mwingine yeyote miongoni mwao kuwa Mwenyekiti wa muda wa Mkutano huo kwa ajili ya shughuli hiyo. Kamati Kuu ya TANDEN inaweza kukutana hata kama viongozi wote wakuu wa chama hawapo.
II: Kazi za Mkutano Mkuu wa TANDEN zitakuwa zifuatazo:-
(1) Kupokea na kufikiria taarifa ya kazi za TANDEN iliyotolewa na kamati Kuu ya TANDEN na kutoa maelekezo ya mipango na utekelezaji wa malengo ya TANDEN kwa kipindi kijacho.
(2) Kuthibitisha, kubadili, kukataa au kuvunja uamuzi wowote uliotolewa na kikao chochote cha chini yake au na mkuu yeyote wa TANDEN.
(3) Kubadili sehemu yoyote ya Katiba ya TANDEN kwa uamuzi wa theluthi mbili za Wajumbe walio na haki ya kupiga kura.
(4) Unapofika wakati wa uchaguzi, Mkutano Mkuu wa TANDEN utashughulikia mambo yafuatayo:-
(a) Kuwachagua Mwenyekiti, Katibu na Mwekahazina wa TANDEN.
(b) Kuunda Kamati za Mkutano Mkuu wa TANDEN kwa kadri itakavyoonekana inafaa.III: Mkutano wa kamati kuu ya TANDEN utakuwa na wajumbe wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa TANDEN.
(b) Katibu mkuu wa TANDEN
(c) Mwekahazina wa TANDEN
(d) Wenyeviti wote wa kamati za TANDEN.
(f) Wawakilishi kutoka Fyn na JyllandIV: Vikao vya Kamati kuu ya TANDEN
(1) Kamati Kuu ya TANDEN itafanya mikutano yake ya kawaida mara moja kila baada ya miezi minne, lakini inaweza kufanya mkutano usiokuwa wa kawaida (dharura) wakati wowote endapo itatokea haja ya kufanya hivyo au kwa maagizo ya kikao cha juu.
(2) Katika mikutano yote ya Kamati Kuu ya TANDEN, uamuzi utafikiwa kwa makubaliano ya jumla, au kwa wingi wa kura za Wajumbe waliohudhuria na kupiga kura. Uamuzi huo ni lazima upitishwe kwa azimio lililoungwa mkono na theluthi mbili ya kura za Wajumbe wote.
(3) Mwenyekiti wa TANDEN atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa kamati Kuu ya TANDEN, lakini Mwenyekiti wa TANDEN asipoweza kuhudhuria, mmoja wa wa viongozi wakuu wa TANDEN atakuwa Mwenyekiti wa muda wa Mkutano huo.V: Kazi za kamati Kuu ya TANDEN
(1) Kuandaa Katiba, Kanuni na kuweka taratibu za kuongoza shughuli mbalimbali
za TANDEN.
(2) Kuandaa Mkutano Mkuu wa TANDEN
(3) Kushughulikia uhusiano kati ya TANDEN na Jumuiya mbalimbali kama vile jumuia za watanzania wanaoishi nchi za nje.
(4) Kutengeneza na kurekebisha Muundo wa TANDEN katika maeneo na nyanja mbalimbali kwa kadri itakavyoonekana inafaa.
(5) Kupendekeza kumsimamisha uongozi kiongozi wa TANDEN iwapo mwenendo na utendaji wake wa kazi vitamwondolea sifa za uongozi. Hata hivyo Mkutano Mkuu wa TANDEN ndio utakaokuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu kumsimamisha uongozi kiongozi wa TANDEN.
(6) Kupendekeza kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote iwapo atashindwa kutimiza masharti ya kuwa mwanachama. Hata hivyo Mkutano Mkuu wa TANDEN ndio utakaokuwa na maamuzi ya mwisho kuhusu kumsimamisha uanachama mwanachama wa TANDEN.VI: Kiwango cha Mahudhurio katika kufikia Uamuzi
Kiwango cha Kura katika kufikia Uamuzi wowote au kujaza nafasi zikiwa wazi ni zaidi asilimia 50 ya wanachama wote.VII: Kujiuzulu Uongozi, Uanachama na Ujumbe wa Kikao
(1) Mwanachama anayetaka kujiuzulu atafanya hivyo kwa kuandika barua ya kujiuzulu kwake na kuipeleka kwa katibu wa chama.
(2) Kiongozi anayetaka kujiuzulu atafanya hivyo kwa kuandika barua ya kujiuzulu kwake na kuipeleka kwa Kiongozi wa chama.
(3) Kwa kutangaza uamuzi wa kujiuzulu kwake mbele ya kikao kilichomchagua.
(4) Mjumbe yeyote wa kikao chochote kilichowekwa na Katiba hii ataacha kuwa Mjumbe wa kikao hicho iwapo hatahudhuria mikutano mitatu mfululizo ya kikao chake
isipokuwa kama ni kwa sababu zinazokubaliwa na kikao chenyewe.
Katiba ya Tanden
Close
Close
Close
Leave a Reply