News

Ripoti ya kikao cha ujio wa Mheshimiwa Balozi Dora Msechu

Ripoti ya kikao cha ujio wa Mheshimiwa Balozi Dora Msechu

Ndugu wana jumuiya,hii hapa ndio ripoti ya ujio wa mweshimiwa balozi wa Dora Msechu,katika kikao kilichofanyika Copenhagen.

RIPOTI YA KIKAO CHA BALOZI WA TANZANIA KWA NCHI ZA SCANDINAVIA NA BALTIC MHE. DORA MMARI MSECHU NA WATANZANIA WAISHIO DENMARK, 21 FEB. 2015

UKARIBISHO

Mwenyekiti wa TANDEN alianza kwa kuwakaribisha Mhe. Balozi na ujumbe wake na kutoa shukrani kwa kutupa fursa ya kukutana na Balozi mpya. Afisa Ubalozi Mr. Jacob Msekwa alichukua fursa ya kumtambulisha Mhe.Balozi Dora Mmari Msechu kwa watanzania walihudhuria kikao hicho mjini Kopenihageni. Afisa alielezea uzoefu wa Balozi na pia uhusiano wa nchi za Scandinavia na Tanzania.

BALOZI:

Mheshimiwa Balozi alianza kwa kushukuru kupata fursa ya kukutana na Watanzania waishio Denmark baada ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mtukufu Malkia Margrethe II tarehe 20 Feb 2015.

Aidha, alishukuru kwa mialiko mbali mbali ambayo tayari ilikuwa imekwisha tumwa toka TANDEN lakini kwa taratibu za kidiplomasia asingeweza kushiriki mikutano hiyo hadi sasa ambapo amekwishawasilisha hati hizo na kuwa mwakilishi rasmi wa Tanzania nchini Denmark. Vile vile alieleza kuwa Ubalozi unafurahi kutumia fursa hiyo kuwafikia Wanzania walio wengi nchini Denmark kwa lengo la kurenew passport zao. Mheshimiwa Balozi alielezea hali ya maendeleo ya kiuchumi na kisiasa nchini Tanzania. Alieleza kuwa Serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete imefanya kazi kubwa kwani uchumi wa Nchi unazidi kukua, miundo mbinu inaimarika, uwekezaji unaongezeka kwa kasi katika sekta mbalimbali za uchumi, na idadi ya watalii inaongezeka siku hadi siku. Viongozi mashuhuri duniani km, Marekani, China, Ujerumani na Kutoka Nchi za Scandinavia wametembelea Tanzania kutokana na Nchi yetu kuwa na mvuto wa kipekee barani Afrika. Hazina kuu ikiwa ni Upendo, Umoja, Mshikamano na utulivu wa nchi yetu, ukomavu wa democrasia na utawala bora. Vile vile Mheshimiwa Balozi alielezea kuhusu hali ya kisiasa nchini na kwamba tarehe 30 Aprili 2015 wananchi wanatarajia kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya na vile vile mwezi Oktoba mwaka huu kutakuwa na Uchaguzi wa Rais Mpya na Wabunge. Alieleza zaidi kuwa masuala haya yanahitaji utulivu hivyo tuiombee nchi yetu. Kuhusu changamoto zinazoikabili nchi yetu kama rushwa, ujambazi, vitendo vyenye mwelekeo wa kigaidi, madawa ya kulevya, ujangili n.k Mhe. Balozi alisema tuzichukulie changamoto hizo kama fursa ya kujiimarisha zaidi katika kuendeleza juhudi za kuzuia na kutokomeza kabisa hali hizo. Mheshimiwa Balozi aliwaomba watanzania wajivunie kuwa ni watanzania na waendeleze mshikamano, ushirikiano na upendo. Mambo muhimu Mheshimiwa Balozi aliyopenda kusisitiza:

  • Upendo na ushirikiano ni siri ya mafanikio.
  • Heshimu sheria za nchi mnazoishi na kwa kufanya hivyo mtaijengea Nchi yetu heshima na sifa nzuri.
  •  Wekezeni Tanzania – Fursa ni nyingi.
  • Tangazeni nchi yetu na vivutio vyake.
  • Dumisheni Umoja miongoni mwenu kwa kuwa Tanzania ni Taifa moja. Aidha, msikubali kubaguana kwa misingi ya dini, itikadi, kabila au rangi kwani sisi ni wamoja.
  •  Msiwe wachoyo wa kupeana siri ya mafanikio yenye manufaa kwa Mtanzania mwenzako k.m fursa za masomo au kazi.

Dumisheni Umoja miongoni mwenu kwa kuwa Tanzania ni Taifa moja.<br /> Aidha, msikubali kubaguana kwa misingi ya dini, itikadi, kabila au rangi<br /> kwani sisi ni wamoja.

Balozi Dora Msechu

Mheshimiwa Balozi alihitimisha maelezo yake kwa kuwakaribisha watanzania waishio Denmark kutembelea Ubalozini Stockholm na kusema Ubalozi ni nyumbani kwenu. Milango ipo wazi .

MASWALI, HOJA NA MAJIBU:

Sehemu hii watanzania walipewa fursa ya kuuliza maswali na kuja na hoja mbali mbali kwa Mheshimiwa Balozi.

1. Watu wanaojiita panya road wanavamia wananchi barabarani?

Jibu: Baadhi ya sehemu nchini kulitokea wahuni waliojiita panya road ambao walianza kufanya fujo ikiwemo kupiga watu lakini Serikali kupitia Jeshi la Polisi lilichukua hatua stahiki na vijana hawa wakadhibitiwa. Hali ya nchi kiusalama kwa jumla ni shwari na wananchi wanataadharishwa wawe waangalifu na habari zinazosambazwa mitandaoni kuhusu matukio kama haya. Kwa mfano, baadhi ya picha zilizosambazwa mitandaoni zimethibitishwa kuwa ni za matukio yaliyotokea miaka ya nyuma na hayahusiani kabisa na panya road.

2. Kuna utaratibu gani wa kupiga kura kwa watanzania walio nje kupiga kura?

Jibu: Utaratibu uliopo sasa unaruhusu kujiandikisha na kupiga kura mtu akiwa Tanzania tu. Hata hivyo, Serikali imeielekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi iangalie uwezekano wa kuwawezesha watanzania wanaoishi nje kujiandikisha na kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka huu kwenye nchi wanazoishi.

3. Diaspora: Kuwekesha nyumbani je kuna urahisi gani kuhusu vibali na sheria?

Jibu: Watanzania waishio Ughaibuni wanashauriwa kuwekeza nyumbani kusaidia maendeleo ya nchi zikiwemo familia zao. Kuna taratibu nzuri za kupata vibali kwa mujibu wa sheria za nchi. Serikali imeanzisha Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Kimataifa na pia hivi karibuni kumeanzishwa Taasisi inayoitwa ”Diaspora Initiative”   vyombo hivi vinajishughulisha na kusaidia watanzania wanaoishi nje kufuatilia masuala yao mbali mbali yakiwemo ya uwekezaji.

Vilevile, Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kutilia maanani urahisi wa upatikanaji vibali na kulinda haki za wawekezaji.

4. Katika mapendekezo ya katiba mpya kuna kifungu kinachohusu wazawa wa Tanzania walio na uraia wa nchi nyingine watapewa kifungu kingine? Urithi, je kuna njia gani za kulinda haki zao mali na urithi? Honorary Consul – DK kuna uwezekano gani kuipata hiyo ofisi tena?

Jibu: Suala la uraia pacha bado liko katika mchakato halijapatiwa ufumbuzi. Suala hili linahitaji pia elimu ya jamii. Katiba mpya inayopendekezwa inatambua uasilia wa mtu yoyote aliyezaliwa kama Mtanzania na Bunge litapewa mamlaka ya kutunga sheria ambazo zitaainisha haki za Mtanzania asilia aliyebadili uraia wake – inatarajiwa kuwa sheria hizo zitajumuisha ustahili wa mtu mwenye uasilia wa Tanzania kupewa hati ya kudumu ya ukazi na haki nyingine nyingi isipokuwa upigaji kura na kugombea uongozi. Kuhusu Ubalozi wa Heshima: Suala hili lipo kwenye mchakato. sifa zake ni awe Raia wa Denmark na asiwe mtumishi wa umma . Awe na mapenzi na Tanzania na awe tayari kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo. Aidha, mtu huyo anatakiwa awe na mikakati mizuri ya kuitangaza Tanzania hasa kwenye fani za biashara na uwekezaji. Wana Diaspora wanahamasishwa kupendekeza majina ya watu wanaoona wana vigezo vinavyofaa kuwa Konseli wa Heshima nchini Denmark.

5. Ubalozi na uwekezaji. Imeonekana kuwa ubalozi uko mbali na suala hilo umezibwa na Wawekezaji? Ziara ya Malkia (2008), Ubalozi haukuwa na taarifa? Ugumu wa kuzitangaza nchi zetu?

Jibu: Ubalozi ulishiriki katika maandalizi ya ziara hiyo lakini haukushirikishwa katika kuandaa ujumbe wa wafanyabiashara wa Denmark walioambatana na Malkia kwenye ziara yake ya Tanzania. Jukumu la kuaanda ujumbe wa Malkia lilikuwa ni la Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark kwa kushirikiana na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania Ubalozi unaendelea na juhudi za kutangaza fursa za biashara na kuhamasisha nchi za Nordic na Baltic kuwekeza Tanzania. Juhudi hizo zimeanzia Sweden ambapo Ubalozi umeshaandaa na kufanya mikutano kadhaa ya uwekezaji kwa ushirikiano na Balozi nyingine za Afrika Mashariki na kwa kushirikisha wana Diaspora . Mipango ipo njiani kufanya mikutano kama hiyo kwenye nchi nyingine ikiwemo Denmark.

6. Elimu ya jamii ni duni nchini mifano ilitolewa inasikitisha na kutisha jinsi akina mama wanavyotesa na kutenda mabaya kwa watoto?

Jibu: Suala la Elimu lina changamoto nyingi ambazo serikali inaendelea kuzifanyia kazi. Serikali imezindua sera mpya ya elimu hivi karibuni ambayo lengo lake ni kuboresha mfumo wa elimu. Msingi mkuu wa sera hii ni azma ya kutoa elimu bure kwa watoto wote, kushirikisha jamii katika kuboresha sekta ya elimu na haki ya kupata elimu kwa jamii yote wasichana, wavulana,walemavu, n.k. Wana Diaspora Denmark wanashauriwa wasaidie katika suala la kuwatafutia vijana wa kitanzania fursa za masomo ya elimu ya juu nchini Denmark na kwingine.

Ubalozi tayari unafanya juhudi za kutafuta fursa za elimu ya juu kwenye nchi za Nordic na Baltic. Zipo nchi mbalimbali zina nafasi za elimu ya juu ambazo watanzania wanaweza kusoma hata kwa njia ya kujitegemea na mfano mzuri ni nchi za Baltic, Estonia, Latvia na Lithuania. Nchi nyingi, zikiwemo za Afrika tayari zina wanafunzi wengi kwenye nchi hizo isipokuwa Tanzania ambayo ina mwanafunzi mmoja tu nchini Estonia. Diaspora pia mtoe mchango wenu kwa kushiriki katika kusaidia kuhamasisha kinga za watoto na haki zao dhidi ya matukio ya ukatili yanaowakumba watoto kwenye jamii yetu.

7. Vitambulisho vya Uraia?

Jibu: Utaratibu unahitaji mtu awepo Tanzania ili kufanya mchakato wa kupata kitambulisho cha uraia lakini Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania (NIDA) imeaanda utaratibu maalum unaohakikisha wana Diaspora wanapata vitambulisho hivyo haraka. Ukiwa Tanzania tembelea Makao Makuu ya NIDA ili upate maelekezo kuhusu utaratibu huo.

8. Swali linahusu uwekezaji wa mashamba na sasa Serikali inadai maeneo hayo yatajengwa sasa ni uwekezaji wa aina ipi?

Jibu: Uwekezaji wa aina zote unakubaliwa hata kilimo maana kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu. Ardhi ni mali ya Serikali ya Tanzania hivyo kama Serikali imeamua kujenga miundombinu kwenye eneo la ardhi yako ya uwekezaji basi utalipwa fidia stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi.

9. Uvamizi mkoani Tanga Mapangoni?

Jibu: Serikali imechukua hatua husika kukabiliana na tatizo hilo. Hili lilikuwa ni tukio la kijambazi lililohusisha kundi la majambazi wiliojificha kwenye pango lililokuwa kilomita 5 kutoka Hifadhi ya Mapango ya Amboni. Polisi wanaendelea na uchunguzi wa suala hili.

10. Filamu zinazoonyeshwa nchini zinachujwa vipi?

Jibu: Hii ni vita ya kimaadili kwenye jamii. Serikali inafanya kila jitihada ikiwa ni pamoja na kuelimisha na kushirikisha jamii katika kupambana na tatizo hili.

11. Suala la Passport za watoto?

Jibu: Watoto chini ya miaka 18 wana haki ya kuwa na passport ya Tanzania lakini inabidi mtoto afikishapo miaka 18, kama ana passport ya nchi nyingine, inabidi achague moja kati ya kukana au kuendelea na uraia wa Tanzania. Aidha, utaratibu sasa unaruhusu watoto wa chini ya umri ya miaka 18 wenye mzazi aliye na asili ya Tanzania kugongewa muhuri wa ukazi wa kudumu(permanent residence) kwenye passport zao za kigeni. Ukiwa Tanzania nenda kufuatilia suala hili kwenye Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kitengo cha Konsula. Hautapata usumbufu wowote.

12. Madawa feki ya hospitali yanayoingia nchini swala linatazamwaje na ni kutoka nchi gani? Wananchi wanapata matatizo na dawa nyingi!’

Jibu: Tatizo linafahamika na vyombo husika vinachukua hatua stahiki kupambana na changamoto hiyo.

13. Tofauti ya maisha ni kubwa mno Tanzania!

Jibu: Tofauti zinazojitokeza kati ya raia maskini na raia matajiri nchini zinazotokana na mabadiliko ya kiuchumi. Hata hivyo, Serikali inaendelea na juhudi za kuboresha maisha ya wananchi wake. Jamii pia hasa wanadiaspora mna nafasi nzuri ya kutoa mchango wenu katika kufanikisha juhudi hizi. Ni vema mkafahamu kuwa kasi ya maendeleo nchini ni kubwa sana.

14. Mijini maendeleo yanaonyesha changamoto la ujenzi?

Jibu: Kuna matatizo mengi ya kujenga bila kufuata taratibu husika za mipango miji lakini Serikali inaendelea na juhudi za kukabiliana na tatizo hili mpaka kufikia hatua ya kubomoa majengo yasiyo na vibali pale inapobidi.

15. Misaada Tanzania imeshapunguzwa kutoka baadhi ya nchi?

Jibu: Nchi za Nordic zinaendelea kuwa watoaji wakubwa wa misaada ya maendeleo kwa Tanzania. Serikali yetu sasa inafanya jitihada za kuimarisha zaidi mahusiano ya kiuchumi kwa kukuza biashara na uwekezaji na hatimae kuwa Taifa linalojitegemea.

16. ELIMU maswali ya nyongeza: a) Elimu ya nchi nzuri Kiswahili kinatakiwa kitumike chuo kikuu ? b) Uwezekano wa kusoma elimu ya juu nchi za nje?

Jibu: Kiswahili ni lugha ya Taifa na ni moja ya lugha kubwa duniani. Mfumo mpya wa Elimu unakipa kipaumbele Kiswahili kama lugha kuu ya mafunzo. Wakalimani bado ni changamoto hivyo watanzania waipende, waikuze na kuitangaza lugha ya kiswahili popote walipo. HOJA: Baadhi ya watanzania walijitokeza kuwa wanaweza kusaidia kuhusu nafasi za elimu ya juu na unesi hapa Denmark. Tuwe wazi kufahamishana na kusaidiana tukisikia nafasi. Scholarship zipo lakini watu wengi hawafanyi juhudi za kuzifuatilia.

17. Swala la Ufisadi?

Serikali inachukulia vipi swala hili? Jibu: Siku hizi uovu na ufisadi unazungumziwa wazi hata Bunge linajadili mapambano na ufisadi na uovu unaanikwa wazi. Mfano ni suala la Escrow ambalo lilijadiliwa kwa uwazi na kutolewa maazimio Bungeni ambayo Rais alishirikishwa kuyafanyia kazi na kutolea uamuzi na taratibu za kuwawajibisha wahusika wa sakata hili kwa mujibu wa sheria bado zinaendelea. Mamlaka husika zinachunguza na kutoa taarifa kwa umma na hoja zote zinajadiliwa kwa uwazi. Nchi za nje zimefurahishwa kuona nchi yetu inaweka wazi maovu na jinsi sakata hili linavyotatuliwa kwa ujumla. Ni muhimu kuiombea nchi yetu iendelee kuwa na amani na utulivu.

18. Swala la kuunganisha vyama vya watanzania katika Nordic na Baltic kwenye sherehe ya uhuru? Mheshimiwa Balozi aliombwa alipokee swala hili na kwa kuwa Denmark ndiyo ya kwanza kutaja hoja hii watanzania wanaomba sherehe ya kwanza ifanyikie Denmark.

Jibu: Ubalozi umelipokea na unaunga mkono suala hilo na unashauri Jumuiya ya Watanzania Denmark iwasilishe mapendekezo Ubalozini ili yafanyiwe kazi kwa ushirikiano na Jumuiya zote za Diaspora hapa Nordic.

 

KUFUNGA KIKAO:

Baada ya masaa zaidi ya matatu kikao kilifungwa na yafuatayo:

Mwenyekiti wa Tanden:

  1. Aliwashukuru Mheshimiwa Balozi na ofisi kwa kutupa fursa ya kukutana nasi.
  2. Mwenyekiti alisisitiza kuhusu ushirikiano na kupeana taarifa.
  3. Watanzania waishio Yullandi wanaomba pia vikao viwe vinafanyika huko mbeleni.
  4. Mheshimiwa Balozi aliwashukuru na kuomba watanzania waendeleze ushirikiano na mshikamano... ”sisi ni ndugu” alisema kwa watanzania.
  5. Ofisa kutoka ofisi ya Ubalozi alieeleza kuwa kazi ya kubadilisha pasiport itaendelea pia jumapili hivyo wote waohitaji huduma hiyo wanakaribishwa.

Ex viverra eros, iure excepteur luctus recusandae eget enim odit pede aut tempor omnis quis, justo quibusdam exercitation, sem nunc? Lobortis, repellat. Aliqua unde natus. Augue nam praesentium ullamcorper veniam hac quas faucibus? Incidunt necessitatibus, error, modi phasellus? Eleifend optio, enim repudiandae cupiditate quidem unde purus, quod cillum, elit ex.

Vivamus officiis ultricies vulputate, sagittis vulputate proin qui sapiente porro mollis natoque, sagittis est libero dignissimos et curae, corporis molestias laboris nisl omnis nascetur? Mollis rhoncus ipsam? Ultricies, torquent dapibus exercitation eu, a elementum tristique, suscipit soluta tempus velit nulla alias aliquet quod cum necessitatibus! Morbi itaque urna, netus labore.

Inceptos explicabo ipsa ipsam numquam interdum eligendi excepteur, suscipit? Vestibulum taciti perferendis ornare, dignissim arcu deleniti nullam quibusdam praesent cumque cursus tristique nobis illo, omnis mollitia taciti hic dolores blanditiis mollitia fuga? Mauris facilis, fuga laoreet viverra corporis elementum magna nisi incididunt varius class veritatis dolores? Aut minus, dapibus itaque.

Suscipit, magni natoque aliquet rhoncus. Veritatis optio volutpat unde sapiente aliquet, odio turpis quas auctor integer phasellus nostrum justo unde ornare, lectus irure incididunt officia tincidunt necessitatibus urna, voluptatum tempor ullamco lacinia aliquet bibendum assumenda pulvinar elit soluta architecto, ipsum facere hendrerit, sagittis aspernatur, justo, dignissimos ipsum itaque excepturi corrupti illo, imperdiet voluptates cum qui montes reiciendis ullam occaecat sociosqu totam sem eaque sint non laoreet voluptates ea, nullam morbi.

Related Articles

The Copenhagen Revival Conference

Leave a Reply

Close
Close

Please enter your username or email address. You will receive a link to create a new password via email.

Close

Close