Chama cha waTanzania waishio hapa Denmark (TANDEN) kushirikiana na shirika la GTS Denmark vimetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya hospitali kuelekea Tanzania,Shinyanga.
- Vitanda vya kulaza wagonjwa (Mashuka,magodoro).
- Magongo ya kusaidia walemavu wa miguu.
- baskeli za kusukumiza za wagonjwa na walemavu.
- Uzio wa kutengenisha sehemu wakati operesheni na sehemu za kulala wagonjwa wodini.
- Scanner ya kuchunguza wa mama wajawazito.
- Vifaa saidizi wakati wa operation ( drip, mipira ya kuwekea dawa, gloves).
Vifaa hivi vyote vinasafirishwa leo kwa njia ya bahari, kuelekea Tanzania ( Shinyanga) kwenye shirika la Agape Aids Control lilipo Shinyanga, ambao ni partner wa TANDEN. Vifaa hivi muhimu katika kusaidia jamii vitasambazwa katika hospital tofauti katika mkoa wa Shinyanga.
Msaada huu/vifaa vimechunguzwa kwa makini kabla ya kuwekwa tayari kwaajili ya safari kuelekea Tanzania na pia TANDEN itasimamia kwa umakini na ufanisi mkubwa katika kuhakikisha msaada huu muhimu unatumika ipasavyo na kufikia walengwa.
Picha za ramani ya Tanzania na Shinyanga tumetoa
By Macabe5387 - Own work, CC BY-SA 4.0, https://commons.wikimedia.org/w/index.php?curid=45569582
By © Sémhur / Wikimedia Commons, FAL, https://commons.wikimedia.org/w/index.php?curid=6686935